BALOZI wa Marekani nchini Korea Kusini anaendelea kuuguza majeraha baada ya kushambuliwa kwa kisu na mtu mmoja mjini Seoul.
Balozi huyo Mark Lippert alishambuliwa na Mkorea Kim Ki-jong mwenye umri wa miaka 55 wakati mkutano wa kuziunganisha tena Korea Kusini na Kaskazini ukuiendelea. Lippert alijeruhiwa usoni na mkononi kwenye shambulio hilo amelazimika kushonwa nyuzi 80 usoni. Mkorea huyo Ki-jong amewahi kufungwa jela mwaka 2010 baada ya kujaribu kumshambulia balozi wa Japan alipokuwa mjini Seoul. Mtu huyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote.
source:clouds
No comments:
Post a Comment