MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) jana aliteta faragha na
Spika wa Bunge, Anne Makinda kushauriana naye kama ajiondoe kwenye
ubunge baada ya chama chake kutangaza kumvua uanachama.
Lakini
pia mbunge huyo jana hiyo jioni alipanga kuonana na spika wa zamani
Samuel Sitta kuzungumza naye kuhusu suala hilo, ambalo habari za uhakika
zinaeleza kuwa amedhamiria kuliaga Bunge hata kabla ya chama chake
kuwasilisha barua ya kumvua uanachama kwa spika.
Akizungumza
na mwandishi jana, Zitto ambaye hakukubali au kukanusha habari hizo,
alisema kwamba atatangaza kujiondoa kwenye ubunge ama la, mara
atakaposhauriana na spika Makinda pamoja na Sitta.
Zitto,
ambaye jana habari zilitapakaa kuwa ataliaga Bunge, alimwambia
mwandishi kuwa habari hizo zinaweza kuwa na ukweli, lakini hatima yake
itajulikana mara atakapokutana na viongozi hao ambao alisema katika
kipindi chake cha ubunge cha miaka 10 walimlea bungeni.
Zitto alisema, “Kama
hizo fununu zipo zitajulikana hivi karibuni, lakini kwanza ni lazima
nishauriane na Makinda na Sitta, hawa wamenilea katika maisha yangu ya
ubunge wakiwa viongozi wangu, hivyo siwezi kufanya jambo lolote
linalogusa ubunge bila wao kushauriana nao.
“Hivi
nakwenda kwa spika nyumbani kwake kwa sababu nina miadi naye na baadaye
nitakwenda kuongea na Sitta…baada ya hapo nitakwambia kitakachofuata,” alisema Zitto.
Zitto
ambaye alifika bungeni jana, alishiriki kikao cha kwa kuuliza swali la
nyongeza na baadaye alishiriki kuchangia kwenye muswada wa sheria ya
kuratibu ajira za wageni nchini.
“Jamani mimi bado ni mbunge si mmeniona nimeshiriki kikao cha leo, hayo mengine yatajulikana baadaye,” alisema Zitto.
Ubunge
wa Zitto utakoma pale chama chake cha Chadema kitakapoandika barua kwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo pia itamwandikia barua spika kumjulisha
kuwa jimbo hilo liko wazi.
No comments:
Post a Comment