Ajali mbaya yatokea leo mkoani Pwani

Tuesday, April 14, 2015

 
Basi la kampuni ya GAMET Trans linalofanya safari zake Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea limepata ajali maeneo ya Kibiti wilaya ya Rufiji-Utete mkoa wa Pwani baada ya kutaka kumkwepa mtu anayedaiwa kuwa na tatizo la ulemavu wa akili,lakini kwa bahati mbaya likamgonga na kufariki papo hapo,taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya ajali hiyo basi hilo liliacha njia na kupinduka na kupelekea kifo cha mtu mmoja aliyegongwa na wengine waliokuwemo ndani ya basi hilo (idadi ya abiria haikujulikana mara moja) kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment