Muhammad Buhari ndiye rais mpya wa Nigeria

Tuesday, March 31, 2015

http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2014/12/11/141211164749_sp_muhammadu_buhari_640x360_ap_nocredit.jpg
Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria jenerali Muhammadu Buhari ameshinda kura za urais na kumuondoa rais aliyeko Goodluck Jonathan mamlakani.
Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan amekwisha mpigia simu mpinzani wake Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.
Hii ndiyo mara kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.
Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa inaonekana kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.
Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.
Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea hao ambao wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile vile kimajimbo .
Wanigeria wengi wamefurahi kuwa hatimaye wameweza kuing'oa mamlakani serikali ambayo haikuwa ikitekeleza majukumu yake kikamilifu.
Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.
Source:bbc

No comments:

Post a Comment