Anyofolewa sehemu za siri na kuliwa na mamba huko Morogoro

Thursday, April 16, 2015

 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Matata Sheba mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro amenyofolewa sehemu za siri na kuliwa na mambo wakati akioga mtoni.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Diwani wa kata ya Tungi, Deogratius Mzeru alisema Sheba alikwenda mtoni kuoga gafla alitokea mamba na kumg’ata.

Alisema wakati Sheba akijaribu kujiokoa kwa kupiga kelele za kuomba msaada alifanikiwa kutoka kwenye maji wakiwa wanavutana na mamba na kelele zilipozidi zilimshtua mamba na kumg’ata korodani na kurudi majini.

“Juzi jioni wakati Shebe anaoga mara alitokea mamba anayeishi katika mto huo na kutaka kummeza lakini katika purukushani alifanikiwa kutoka nje ya maji lakini alikuwa ameng’atwa sehemu zake za siri ”Mzeru.

Alisema baada ya taarifa hizo kumfikia aliamua kutafuta usafiri wa kumpeleka hospitali ambapo hali yake ilikuwa mbaya.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Rita Lyamuya alisema hali ya mgonjwa imekuwa ikiimarika ingawa bado ana maumivu.

Source:swahilimagazine.com

No comments:

Post a Comment