Mnyama wa ajabu agunduliwa Tanzania

Wednesday, April 1, 2015

 
Kwa mara ya kwanza askari wa wanyamapori katika mbuga ya Serengeti nchini Tanzania wamemgundua mnyama huyu waliyempa jina la "Tembomilia" na wanasayansi wanasema ni mara ya kwanza kwa kiumbe cha aina hii kuonekana duniani. Hivi sasa walinzi hao wa wanyamapori na wanasayansi wanamuhifadhi mnyama huyu wa ajabu, ambaye wanasayansi tayari wamempa jina la kitaalamu la "Tembomilia Tanzanianicus". Jina lenyewe la "Tembomilia" linatokana na maneno ya Kiswahili "tembo" na "pundamilia". Tembomilia aliyegunduliwa sasa ni wa dume akiwa na umri unaokisiwa kuwa miaka miwili na uzito wa kilo 520. 
source:DW

No comments:

Post a Comment