Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza amejerea nyumbani. Mapigano mukubwa yatokea

Thursday, May 14, 2015


Image result for Pierre Nkurunziza
Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amejerea nyumbani hapo jana, baada ya kuwepo kwa jaribio la kumpindua akiwa nchini Tanzania kuhudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwa wakijadili mgogoro wa Burundi.
Maafisa wa serikali wanasema kurejea nyumbani kwa Rais huyo sasa ni ishara kuwa jaribio la kumpindua limeshindikana.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Niyongabo amesema vikosi vya serikali ya Burundi vimefanikiwa kudhibiti hali ya mambo na kuzima jaribio la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza.
Tayari vikosi vya serikali vimetia nguvuni baadhi ya wanajeshi waliokuwa wakijaribu kuipundua serikali huku baadhi yao wakijitetea kuwa walirubuniwa.
Hapo jana kulikuwa na mapigano makali karibu na radio ya taifa kati ya majeshi 
yaliyojaribu kuipindua serikali na yale yanayomtii Rais Pierre Nkuruziza.
source:bbc

No comments:

Post a Comment